Post Code : P.O BOX 3000 - 80100 MOMBASA
March 2025
2:0 minute
Exam code: 451232
1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
3. Jibu maswali yote.
4. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
6. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1 | 2 | 3 | 4 | Total |
---|---|---|---|---|
Jibu maswali yote
UFAHAMU (alama 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu Maswali
Ulimwengu mzima ulisimama ghafla na shughuli za kawaida zikakwama katika mataifa yote duniani. Walimwengu walipata kibarua kigumu mno huku shughuli za uchukuzi wa kimataifa zikitatizika kwa njia zisizomithilika. Ikumbukwe pia kuwa masomo yalitatizika pakubwa huku viwango vyote vya shule vikifungwa.
Vituo vya afya navyo vilifurika kwa msongamano mkubwa wa watu huku wahudumu wa afya wakilemewa na idadi kubwa ya wagonjwa. Wahudumu hao walijipata kwenye wadi na vyumba vya wagonjwa mahututi na wengine wengi walifariki . Wengineo walikosa nafasi ya matibabu au ya kulazwa katika hospitali walizohudumu.
Uchumi uliathirika pakubwa. Watu wengi walipoteza kazi zao. Wengine walitumwa nyumbani kwa likizo bila malipo nao wengine wakikatwa mishahara kwa asilimia kubwa. Biashara nazo hazikusazwa na gonjwa hili kwani nyingi zilifungwa wengine wakipata hasara chungu nzima. Benki zilijipata kwa njia panda kwa wateja kushindwa kulipa mikopo.
Usisahau kuwa maelfu ya watu walipoteza maisha yao huku wengine wengi wakiendelea kukabiliana na makali ya ugonjwa wa Covid-19 ambayo kwa sasa ni uhakika kuwa umejua kuwa ndio ninaozungumzia. Kenya, kama mataifa mengine ulimwenguni inaendelea kukabiliana na janga hili.
Miongoni mwa dalili za mapema za maambukizi ya gonjwa hili ni kukohoa, kushindwa kupumua au ugumu wa kupumua, joto jingi au baridi kali mwilini, maumivu ya misuli au mwili, kutapika au kuendesha, kupoteza hisia za kuonja na kunusa miongoni mwa mengine. Yeyote anayeonyesha dalili hizi anashauriwa kujitenga na kwenda hospitalini mara moja.
Ni muhimu kujilinda dhidi ya virusi hivi. Vaa barakoa kila wakati unapoenda kwenye watu. Kumbuka kuosha mikono yako kwa maji yanayotiririka na sabuni au kuitakasa. Epuka mikusanyiko ya watu na uzingatie umbali wa mita moja unapokumbana na watu. Kaa nyumbani kama inawezekana. Wenye magonjwa mengine kama shinikizo ya damu, ukimwi, saratani, kisukari miongoni mwa mengine na pia watu wenye umri wa juu wanashauriwa na wataalamu wa afya wawe makini zaidi kwani wamo hatarini zaidi.
Hebu tugeukie mikakati mbali mbali iliyowekwa na serikali ya Kenya tangu kuliporipotiwa kisa cha kwanza nchini. Serikali ilitangaza kufungwa kwa shule. Kando na kufungwa huko, kafyu ya saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi iliwekwa hapo awali, hatua iliyolegezwa baadaye. Kufungwa kwa uchukuzi wa kimataifa ulitangazwa huku uchukuzi nchini ukidhibitiwa kwa kupunguzwa kwa idadi ya watu kwenye uchukuzi wa uma. Mikusanyiko ya watu ulipigwa marufuku nazo kanisa zikifungwa japo kwa muda. Idadi ya watu katika arusi na mazishi ilipunguzwa mno. Maeneo ya burudani pia yalifungwa kwa muda nayo maeneo ya maabadini yalifungwa miongoni mwa mikakati mingine.
Baada ya miezi kadhaa, makali ya janga hili tandavu yalizidi kuwakumba wakenya huku kufungwa kwa nchi kukiendelea kuathiri shughuli ya kawaida za kujikimu. Serikali iliweka mikakati ya kuinua uchumi. Wakenya wa viwango vya chini walitumiwa pesa za kujikimu huku wafanyibiashara wadogo wakiinuliwa kwa mikopo. Serikali pia ilizirai benki kuzungumza na wadeni wao na kuwasogezea nyakati za kulipa. Ikumbukwe pia serikali ilipunguza au kuondoa ushuru kwa Wakenya wenye kipato cha chini. Serikali pia ililazimika kulegeza mikakati kadhaa ili kuwapa Wakenya nafasi ya kujichumia. Saa za Kafyu zilipunguzwa huku uchukuzi wa kitaifa na kimataifa ukifunguliwa upya. Shule pia zilianza kufunguliwa japo kwa watahiniwa. Wamiliki wa maeneo ya burudani walinufaika na kufunguliwa kwa maeneo hayo. Viongozi wa kidini na wafuasi wao walikuwa na kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali kuwafungulia maeneo ya kuabudu.
Wakenya wanaendelea kuhimizwa kufuata kanuni za wizara ya Afya dhidi ya Covid -19. Hii inaendelea huku Wakenya wakilaumiwa kwa kutovaa barakoa, kuendelea kutangamana katika mikutano ya kisiasa, kutoosha wala kutakasa mikono, kutozingatia saa za kafyu miongoni mwa mengine.
Ulimwengu unaendeleza mchakato wa kutafiti na kutafuta chanjo ya korona huku baadhi ya mataifa yakitangaza kupiga hatua kubwa na kwamba tutakwamuliwa hivi karibuni. Kujilinda kunabaki kuwa chanjo kuu.
Maswali
a. Thibitisha kwamba Covid-19 umezuia utangamano wa kimataifa. (Alama 1)
.......................................................................................................................................................

b. Eleza kinaya inayojitokeza kwa Covid-19 na wahudumu wa afya. (Alama 1)
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
c. Covid -19 imesababisha madhara mengi ya kiuchumi. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja tatu. (Alama 3)
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
d. Taja dalili zozote mbili za maambukizi ya virusi vya korona. (Alama 1)
......................................................................................................................................................
.......................................................................................................................................................
e. Eleza matendo matatu kulingana na kifungu hiki ambayo yanamweka mtu kwenye hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu (Alama 3)
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
f. Taja mikakati miwili iliyowekwa na serikali ya Kenya kukabiliana na virusi hivi. (Alama 2)
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
......................................................................................................................................................
g. Serikali ya Kenya ililegeza mikakati yake vipi? (Alama 1)
......................................................................................................................................................
h. Eleza maana ya maneno yafutayo jinsi yalivyotumika kifunguni (Alama 2)
i) Kafyu
......................................................................................................................................................
ii) Mchakato
......................................................................................................................................................
UFUPISHO (alama 15)
Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, kumekuwa na mfumko wa bei ya bidhaa muhimu hivi kwamba idadi kubwa ya raia wanalala njaa.Uchunguzi uliofanywa na mashirika ya kijamii kuhusu bei ya bidhaa hizo umeonyesha kuwa familia za kawaida zinatumia nusu ya mapato yao kununua chakula .Bila shaka yoyote,hili ni janga linaloendelea kutokota .Tunafahamu kuwa kupanda kwa bei ya petroli kimataifa kumechangia kuongezeka kwa bei hiyo ya vyakula ,kwa namna moja au nyingine.
Mbali na vyakula ,gharama ya kupangisha nyumba,maji,stima na mafuta imepanda kwa muda wa miezi sita iliyopita kati ya Februari na Julai 2022. Kwa mujibu wa Benki ya dunia, kupanda kwa bei ya vyakula kumesukuma familia nyingi katika lindi la umaskini.
Ingawa serikali haina uwezo wa kuthibiti baadhi ya sababu zinazochochea kuongezeka kwa bei ya vyakula nchini,haipaswi kutulia tuli ikisubiri suluhisho litokee kisadfa. Inasikitisha kwamba viongozi wetu wanatumia muda mwingi kuchapa siasa huku raia wa kawaida wakiendelea kuumia. Iweje basi kwamba katika vikao vyao vya hadhara wanasiasa wanatumia muda mwingi kuzungumzia maswala ya kugawana wananchi na kufichua njama za kuwaangamiza wapinzani wao badala ya kueleza namna watakavyokabiliana na janga lililopo la njaa.Ni lini watafahamu kwamba huwezi kumtawala mtu mwenye njaa.
Kwa muda mrefu ,baa la njaa limekuwa likihusishwa na maeneo ya kaskazini mwa nchi yetu; lakini kama uchunguzi ulivyoonyesha, familia nyingi nchini zinaumia na wengi hawawezi kumudu bei ya bidhaa muhimu kama sukari ,unga,mafuta ya kupikia na kadhalika.
Wakati umewadia kwa serikali kuchukua hatua madhubuti kwa kuwa, kama ilivyo ,ni vigumu kumtawala mtu aliye na tumbo tupu na mbaye hajijui wala hajitambui kuhusu atakapopata lishe.
MASWALI
(a) Ukizingatia taarifa uliyosoma, fafanua athari za mfumko wa bei kwa wananchi. (alama 5) (maneno 35)
MATAYARISHO
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
MAJIBU
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza mambo muhimu anayoyazungumzia mwandishi katika aya za mwisho nne. (Maneno 55-60) (alama 10)
MATAYARISHO
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
MAJIBU
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
MATUMIZI YA LUGHA.(alama 40)
a) Taja ala zinazotumiwa katika sauti zifuatazo. (alama 1)
(i) dh..........................................................................................................
(ii) m.............................................................................................................
b) Unda neno lenye sauti zifuatazo (alama 1)
kipasuo sighuna cha midomoni,irabu ya mbele juu,kitambaza, irabu ya mbele juu
………………………………………………………………………………………………..
c) Tofautisha shadda na kiimbo (alama 2)
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
d)
i)Mofimu ni nini? (alama 1)
…………………………………………………………………………………………………..…………………………………………………………………………………………………..
ii) Tambua mofimu katika fungutenzi hili (alama 3)
kilichoangukiwa
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
e) Tumia nomino za aina ulizopewa katika sentensi moja. (alama 2)
(i) nomino mahususi.
(ii) nomino ya wingi.
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
f) Tunga sentensi sahihi na ubainishe kiima na kiarifu. (alama2)
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
g) Fuata maagizo:Wanafunzi walitosheka na chakula (alama 2)
Anza kwa : Chakula………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
h) Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi. (alama 4)
Askari jela amefikishwa mahakamani.
i) Tumia ngeli ya ku- katika sentensi ya wingi. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
j) Tunga sentensi na uonyeshe kirai nomino, kirai kivumishi na kirai kielezi (alama 3)
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
k) Onyesha matumizi mawili ya herufi kubwa (alama 2)
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
l) Andika katika ukubwa. (alama 2)
Mji huu una watu wengi.
…………………………………………………………………………………………………..
m) Kanusha sentensi ifuatayo (alama 2).
Mwanafunzi akitia bidii atapita mtihani
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
n) Bainisha matumizi ya ‘na’ katika sentensi ifuatayo (alama 2)
Askari na jambazi wana silaha kali.
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
o) Tunga sentensi moja kutofautisha vitate vifuatavyo. (alama2)
i) Mji
ii) Mchi
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
p) Andika katika kinyume (alama 1)
Juma alimwoa Frida mwaka jana.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
q) Andika katika usemi wa taarifa (alama 2)
“Hamjambo wanafunzi wangu,”mwalimu alisema.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
r) Tungia kiunganishi ‘maadamu’ sentensi sahihi (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
s) Eleza maana ya misemo ifuatayo. (alama 2)
(i) kupiga domo……………………………………………………………
(ii) kupiga kijembe………………………………………………………….
ISIMU JAMII (ALAMA 10)
Mhusika.
X : Hebu sema majina yako kamili?
Y : Mussa bin Maksuudi.
X : Ulisema unataka kukata rufani? Kulingana na kifungu sheria nambari 2 (a), una haki hii.
Y : Ikiwezekana mheshimiwa.
X : Usitie shaka umepata presidential amnesty.
Y : Alhamdulillahi, Nitaenda Msikitini Ijumaa kuabudu na kumshukuru Mungu.
Maswali
(a) Tambua muktadha wa mazungumzo haya. (alama.2)
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..........
(b) Tambua wahusika (alama 2)
X……………………………………………………………………………………………
Y……………………………………………………………………………………………
(c) Eleza sifa zozote sita za lugha inayotumika katika mazungumzo haya. (alama.6)
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………