Post Code : P.O BOX 3000 - 80100 MOMBASA
March 2025
2:0 minute
Exam code: 81109
1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
3. Jibu maswali yote.
4. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
6. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1 | 2 | 3 | 4 | Total |
---|---|---|---|---|
Jibu maswali yote
UFAHAMU (alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Haikuwahi kunija akilini kuwa jambo kama hilo lingeweza kunikumba.Lilinipata kwa kasi sana.Nilididimia katika luja.Maisha yangu ya baadaye yalielekea kuingia giza kuu na kuniauni hakuwepo.
Nilikulia katika Kijiji cha Mwanda na wazazi wangu na mnuna wangu. Hatukuwa matajiri lakini hatukukosa mahitaji ya kimsingi. Wazazi wangu walinikumbusha kila mara nitie chudi masomoni ili angaa Maisha yangu ya mbeleni yawe mazuri kuliko yale niliyokulia.
Nilipojiunga na Shule ya Upili ya Kazana sikuwa na marafiki wengi. Nilianza vyema lakini nilipoingia kidato cha pili Maisha yangu yalichukua mkondo mwingine. Sikushiriki katika michezo yoyote au chama chochote cha wanafunzi. Nikuwepo tu! Hali hii iliniletea upweke mkuu nami nikatafuta jinsi ya kujaza ombwe hilo.
Nakumbuka likizo ya muhula wa pili vyema. Nilialikwa karamu na Rafiki yangu mmoja aliyeishi karibu na kwetu. Karamu yenyewe ilikuwa ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Karamuni, wengi walionekana kufahamiana na walipiga gumzo kwa uchangamfu. Vicheko vilihizinika katika gumzo yao.Mimi nilbaki na upweke wangu.
Baadha ya vyakula na vinywaji kwisha, muziki uliwekwa na vijana wakaanza kusakata densi. Mabanati wengi walinengua viuno nusura wakatike nyonga . Mvulana alinijia kujitambulisha kwa jina Todi. Alikuwa na maneno mengi kama chiriku.Alikuwa natafuna mairungi na mara kwa mara alikuwa akitia vidonge fulani na kuvitafuna . Anieleza kuwa vidonge hivyo vilikuwa vinampa uchangamfu wa ajabu.
“Je, ungetaka kuvijaribu”Aliniuliza.
Kwanza nilidinda lakini akanishi na nikakubali. Alinipa vidonge viwili na chingamu. Niliifungua chingamu na nikaanza kuitafuna. Nikaweka kidonge cha kwanza mdomoni na nikatafuna vile vile. Hakikuwa na ladha chungu kama nilivyotarajia. Nikatia kidonge cha pili mdomoni nacho pia nikakitafuna.
Muda wa nusu saa uliisha nami nikaanza kuhoji ikiwa vidonge vilikuwa na athari yoyote. Fikira zile ni kama zilichochea vidonge hivyo kuanza kazi. Nilihisi kichwa change kikiwa chepesi. Mwanga wa taa uakaongezeka na utamu wa muziki ukakolea. Nilipenda jinsi nilivyohisi .Nilitamani kujihisi hivyo milele!
Uraibu wa kutumia dawa za kulevya ulianzia hapo.Nilivuta bangi , nikatumia kokeni na ketamine. Sikufikira nilikuwa katika hatari yoyote. Masomoni nilianza kushika mkia na kuchekwa na wnafunzi wengine. Nilijitafutia nafuu ya muda katika dawa za kulevya.
Jumapili moja nilialikwa na rafiki yule yule kwao. Wazazi wake walikuwa wamesafiri
Naye akaachwa nyuma ili alinde nyumba yao. Ilikuwa asubuhi na tuilkuwa na siku nzima ya kujitawala kwani wazai wake wangerudi jioni. Waama paka akiondoka panya hutawala.Tulikuwa na mihadarati ya aina aina; si heroini, si kokeni. Si bangi, si pombe; tulitaka kujaribu yote.Tulichanganya yote.
Sikumbuki yote yaliotokea.Nakumbuka tu nilitapika na baadaye nikapoteza fahamu. Nilisimuliwa baadaye kuwa wenye nyumba walirudi na kutupata tu hali mahututi; si wa maji si wa chakula. Waliita ambulensi na kutukimbiza hospitalini.Nilipopata fahamu nilijipata kitandani ndani ya chumba chenye kuta nyeupe .Wazazi wangu na mdogo wangu walikuwa wamesimama kando ya hicho na nyuso zao zilionyesha fazaa kuu. Ilikuwa wazi kuwa nilikuwa nimewasaliti upeo wa kusaliti. Machozi anilengalenga . Nilitamani ardhi ipasuke inimeze mzimamzima niondoke na aibu iliyonikabili.
Muuguzi aliingia na kuvunja kimya kilichotawala chumba kile.”Huyu na rafikiye waliponea chupuchupu ,”aliwaambia jamaa zangu. Aliongezea kuwa ikiwa nilithamini Maisha yangu sikuwa na budi kuepukana na matumizi ya dawa za kulevya.
MASWALI
a) Kwa nini msimulizi alkiumbwa na upweke alipojiunga na shule ya upili? (alama 3)
b) Eleza sifa moja ya msimulizi iliyomfanya ashawashike kuingilis mihadarati.(alama 1)
c) Eleza madhara yaliomkumba msimulizi katika matumizi ya dawa za kulevya.(alama 2)
d) Eleza sifa mbili za Todi.(alama 2)
e) Toa mifano miwili miwili ya mbinu zifuatazo kutoka kwenye ufahamu(alama 4)
i) Utohozi
ii)tabaini
f) Eleza maana ya maneno na mafungu yafuatayo kama yalivyotumika katika ufahamu .(alama 3)
i)nitie chudi
ii)tuja
iii)fazaa kuu
MUHTASARI(ALAMA 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali;
Ni dhahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni.Janga hili limeshamiri hususan pembeni mwa bara la Afrika na kanda za Affrika Mashariki .Taarifa za uharamia zimetawala vyombo vya habari , kiasi kwamba haipiti siku bila kuripotiwa visa vipya vya matendo haya mabovu ambayo yanaweza tu kumithilishwa na uhayawani.Matukio haya yamewalimbikizia mabaharia wa nchi husika , simanzi na masaibu yasioweza kutiwa mizani.
Yamkini tatizo hili halitokei pasi na kumotishwa na kitita kikubwa cha fidia kinachodaiwa na maharamia hawa.Aghalabu , suala hili lahusishwa pakubwa na azma na ari ya kuendeleza ujambazi wa kimataifa sawia na ulipuaji wa bomu mjini Nairobi na Dar-es-saalm mnamo Agosti 7,1998 na tukio la Septemba 11. Mwaka wa 2001 kule Marekani.Maafa na uharibifu wa mali si hoja , la mno kwa maharamia ni kutosheleza matakwa yao. Kwa upande mwingine, ukosefu wa tawala-wajibika katika maeneo kunatokea unyama huu ni thibitisho tosha la mazingira yanayowezeha na kuruhusu kuchipuka wa janga hili.
Mchipuko wa baa la uharamia umelengewa jamii ya kimataifa ambayo ni mhdumu mkuu wa harakati za kusitisha majanga makubwa kama vile njaa, umaskini na magonjwa yaliosheheni pakubwa barani.Bila shaka , hili suala linalosawisishwa na ‘kinyume mbele’.Maharamia wanatishia utangamano wa kimataifa wanapotibua usafiri wa abiria na shehena zinazoelekezwa sehemu tofauti ulmwenguni.
Matumizi ya kidiplomasia na mashauriano hayaelekei kuzalisha matunda katika juhudi za kudhibiti uharamia. Zaidi ya hayo , matumiz a nguvu yahusishayo mashambulizi pamoja na maharamia kufunguliwa mashtaka nchini Kenya na Ufaransa kunaelekea kuzipiga jeki juhudi za uharamia ulimwenguni. Aidha, utawala wan chi kunapochipuka uharamia haujajizatiti kuharamia doa hili linalotisha ustawi wa kimataifa.
Mathalan, ni jambo lisilopingika inapobainika kuwa uharamia umedumaza biashara ya kimataifa hali inayochangia upungufu na ucheleweshaji wa bidhaa muhimu zinazoendeleza ustawi wa uchumi. Dosari hii inaelekea kukwamiza mojawapo wa maendeleo ya milenia yanayosisitiza uimarishaji na ushirikiano wa maendeleo na upanuzi wa masoko ulimwnguni.Harakati za kikatili katika kanda mashariki ya bara Afrika zimejuhumiwa.Ni muhali kuwa utalii kustawi kwenye maeneo yalio na tishio la usalama. Itakumbukwa bayana kwamba watalii hawasafiri tu kwa ndege bali hata kwa meli.
Jitihada za kuweka laini za mawasiliano chini ya bahari ili kurahisha na kupunguza gharama za mtandao ulimwenguni ni ndoto ambayo haijatimia hadi hivi sasa, kufuata juhudi za maharamia katika Bahari Hindi. Kwa mujibu wa hali hii , mawasiliano mepesi na nafuu yasitarajiwe hivi karibuni.Licha ya hayo , shughuli za uvuvi na biashara nnyinginezo kwenye kanda ya mwambao zimetiliwa shaka si haba.
Itabidi mikakati kabambe na suluhisho la kudumu liweze kupatikana ili vitendo vya uharamia viweze kusitishwa.
a) Fupisha aya mbili za kwanza kwa maneno 50. (alama 6)
Matayarisho
Nakala safi
b) Onyesha jinsi ambavyo Kenya imeathiriwa na uharamia na namna hali hii iantia hofu kwa maneno 50. (alama 5)
Matayarisho
Nakala safi
c) Fupisha aya mbili za mwisho kwa maneno 40. (alama 4)
SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA( ALAMA 40)
a) Andika maneno yoyote yanayoanza na kwa sauti zifuatazo;(alama 2)
i) Kitambaza na irabu ya chini…………………………..
ii) Kizuiwa ghuna cha masine na kiwamizo hafifu cha koromeo……………………….
iii) Kiyeyusho cha mdomo na irabu ya nyuma wastani……………………………………………………
iv)Kimadende na irabu ya mbele juu……………………………………………………………………………
b) Tambua kiimbo;Tafadhli niazime kalamu yako kwa muda. (alama 2)
c) Andika maneno yalio na miundo ifuatayo;(alama 2)
i)Kiambishi cha umoja , mzizi, kiishio –o
ii)kirejeshi cha umoja , kiambishi cha mahali
d) Unganisha sentensi zifutazo ili uweze kuunda sentensi ya masharti;(alama 2)
Wanasayansi watatabiri mapema.
Wanasayansi watafaulu kuondoa majanga
e) Tunga sentensi kwa kutumia nomino kama kivumishi.(alama 2)
f) Andika sentensi inayoanza kwa kiima na kumalizika kwa kijalizo.(alama 2)
g) Badilisha shamirisho kitondo kuwa shamirisha kipozi katika sentensi uliopewa. (alama2)
Mtoto wa Juma amefundishwa virai kwa kutungiwa sentensi za virai.
h)Tunga sentensi yenye kirai nomino, kirai kitenzi na kirai kielezi(alama3)
i)Andika katika hali ya ukubwa;Mtoto huyu amevaa kiatu kikubwa.(alama 3)
j) Kanusha;Mama hucheka sana akifurahi.(alama 1)
k)Akifisha;jichunge akasema musa msimamo wako huenda ukakuathiri sana.(alama 2)
l) Changanua kwa njia ya mshale;(alama 4)
Juma alichoka sana alipokuwa akifanya mazoezi jana jioni.
m) Tunga sentensi mbili kudhihirisha maana mbili za neno katia. (alama 4)
n) Andika vinyume vya maneno yaliopigiwa mstari;
Mwanafunzi jasiri hujitahidi katika masomo yake.(alama 2)
o) Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo;(alama 2)
Kila darasa likipunguza kiwango cha kelele idadi ya wanafunzi wanaofaulu wataongezeka.
p) Kwa kutolea mfano katika sentensi elezea matumizi mawili ya kiambishi -ki.(alama 2)
q) Onyesha uamilifu wa viambishi katika neno lifuatalo;Walilana(alama 2)
r) Tofautisha aina mbili za mofimu.(alama 2)
ISIMU JAMII(ALAMA 10)
Eleza sifa kumi za lugha utakayotumia ukipata nafasi ya kutangaza mchaezo wa kandanda. (alama 10)