Name
Adm no
Class
Signature
Date
School
DIJIPLEX SECONDARY SCHOOL

Post Code : P.O BOX 3000 - 80100 MOMBASA

KISWAHILI KIDATO CHA TATU

FORM 3 : TERM 1 2025

March 2025

2:0 minute

Exam code: 91102

Instructions to Candidates

1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.

2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.

2. Jibu maswali manne pekee.

3. Swali la kwanza ni la lazima.

4. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani:

Ushairi, Riwaya, Tamthilia, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi.

5. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

6. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

For Examiner's Use Only

MASWALI
1 2 3 4 5 6 7 8 Total

MASWALI

 Jibu maswali kulingana na maagizo

1. 

FASIHI SIMULIZI

Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali

Mimi ni Olichilamgwara

Olichilamgwara mwana mbee wa Ojilong

Ojilong wa Marukatipe

Wazee waliposhindwa

Nilivuka misitu milima na mito

Ni mimi jabali

Kipande cha jifya la mama

Nilipokuwa nalisha mifugo

Nilisikia baragumu inalia

Baragumu ya wito

Mifugo wa mtemi wamechukuliwa

Nikachukua mkuki wangu

Wenye kigumba cha mti

Nikachukua upanga wangu

Wenye makali kama mmweso wa radi

Upanga uliopasua pembe za nyati kwa dhoruba moja

Ndipo nilipofyatuka kasi kama umeme

Kufumba kufumbua nikawakaribia nduli

Kusikia vishindi vyangu wakaanza kubabaika

Kuona kifua changu cha manyoya ya kanga wakatetemeka

Macho yangu makali kama kaa la moto yalipowatazama wakakimbia

Mkuki wangu ulipaa kama umeme

Wote wakalala

Mifugo wakanifuata…

Mko wapi vijana

Mmekuwa kama majivu baada ya moto kuzimika?

 

Maswali

a) Tambua kipera ulichokisoma na udhibitishe jibu lako                   (al. 2)

 

 

 

b) Tambua sifa za jamii zinazosawiriwa katika utungo huu                         (al. 2)

 

 

 

 

 

c) Kwa kutoa mifano bainisha vipengele vine vya kimtindo vilivyotumika       (al  4)

 

 

 

 

d) Fafanua sifa nne za kipera hiki                               (al. 4)

 

 

 

 

e) Eleza mambo manne ambayo mtendaji wa kipera hiki anaweza kufanya ili kufanikisha utendaji wake.                               (al. 4)

 

 

 

 

 

 

f) Fafanua mikakati ambayo jamii inaweza kutumia ili kuzuia tungo kama hizi kufifia (al. 4)

 

 

 

 

2. 

      USHAIRI

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali:

Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki,

Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki

Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

 

Wengine watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo,

Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakazifuata nyago,

Hadi kwenye wao ua, pasipo hata kupesa, wala kukupa kisogo,

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka

 

Pindi kinunua kitu, hafurai Shaitani, bali tajawa chukizo,

Mtu kiwa mtukutu, tanunua mtimani, kwalo lako tekelezo,

Tamko lake ‘Subutu’, kuondoa tumaini, na kukuulia wazo,

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka,

 

Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai,

Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui,

Hana faida nyumbani, ni mtu akuchimbaye, mradi usitumai,

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka,

 

Kwa hakika ni balaa, kumkirimu mchawi, aliejaa uchoyo,

Bahati ina hadaa, kukupa alo sadawi, aibatili rohoyo

Mipangoyo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza vunja kaniyo,

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka

 

Ninacho change killo, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa,

Ningetoa azimio, lakini uwezo sina, kwa matatizo kuambiwa,

Ama nitumie mbio, fuadi ninanena, akilini nazuiwa,

Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.

 

 

MASWALI:

a) Lipe shairi hili anwani mwafaka.                                                           (alama 1)

 

 

b) Fafanua mambo matatu ambayo nafsineni analalamikia.                       (alama 3)

 

 

 

 

c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo.                     (alama 3)

(i) Idadi ya vipande katika kila mshororo

 

 

(ii) Mpangilio wa vina katika kila ubeti

 

 

(iii) Idadi ya mishororo katika kila ubeti

 

 

d) Andika ubeti wa nne katika lugha nathari.                                             (alama 4)

 

 

 

 

 

 

e) Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili.    (alama 2)

 

 

 

f) Huku ukitoa mifano, onyesha mbinu mbili alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi.                               (alama 2)

 

 

 

g) Andika aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili.            (alama 2)

 

 

 

h) Fafanua muundo wa ubeti wa tano.                                            (alama 3)

3. 

               USHAIRI

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

Ee mpwa wangu,

Kwetu hakuna muoga,

Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo,

Fahali tilichinja ili uwe mwanamume,

Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu!

Iwapo utatingisa kichwa,

Uhamie kwa wasiotahiri.

 

Wanaume wa mbari yetu,

Si waoga wa kisu,

Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo,

Wewe ndiye wa kwanza,

Iwapo utashindwa,

Wasichana wote,

Watakucheka,

Ubaki msununu,

Simama jiwe liwe juu

Ndege zote ziangamie.

 

Simu nimeipokea,

Ngariba alilala jikoni,

Visu ametia makali,

Wewe ndiye wangojewa,

Hadharani utasimama,

Macho yote yawe kwako,

Iwapo haustahimili kisu,

Jiuzulu sasa mpwa wangu,

Hakika sasa mpwa wangu,

Hakika tutakusamehe, mwaka kesho unakuja.

 

Asubuhi ndio hiii,

Mama mtoto aamushwe,

Upweke ni uvundo,

Iwapo utatikisa kichwa.

Iwapo wewe ni mme,

Kabiliana na kisu kikali,

Hakika ni kikali!

 

Kweli ni kikali!

Wengi wasema ni kikali!

Fika huko uone ukali!

Mbuzi utapata,

Na hata shamba la mahindi,

Simama imara,

Usiende kwa wasiotahiri.

 

Maswali

a) Hili ni shairi la aina gani? Thibitisha                                      (al. 2)

 

 

 

 

b)  Tambua anayeimba na anayeimbiwa shairi hili      (al. 2)

 

 

 

c)  Toa ithibati kwenye shairi hili kuthibitisha kuwa msimulizi ana taasubi za kiume (al. 2)

 

 

 

d)  Taja kwa kutolea mifano mbinu zozote nne za uandishi katika shairi hili           (al. 4)

 

 

 

 

 

e)  Taja shughuli zozote mbili za kiuchumi za jamii inayorejelewa katika shairi hili      (al. 2)

 

 

 

f) Eleza mbinu alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiuarudhi              (al. 4)

 

 

 

 

 

g) Msamiati ufuatao umetumika kwa maana gani katika shairi hili?                 (al. 4)

          i)    Mbari

 

          ii)    Msununu

 

          iii)   Ngariba        

 

          iv)   Uvundo

 

4. 

TAMTHILIA; BEMBEA YA MAISHA – TIMOTHY M. AREGE

 “Huku ndiko kuvumilia hasa. Tazama faraja ilivyoalika sasa”

a) Weka dondoo hili katika muktadha.                                                      (alama 4)

 

 

 

 

 

b) Eleza sifa za msemaji katika dondoo.                                                   (alama 6)

 

 

 

 

 

c) Onyesha jinsi faraja ilivyoalika katika maisha ya msemewa kwa kurejelea tamthilia ya: Bembea ya Maisha.                                                              (alama 10)

5. 

 (a) Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho.                                     (alama 10)

 

Maskini mke wangu! Kumbe ugonjwa haukumsaza mwaka baada ya mwaka. Umemla bila huruma. Awali niliona kama mchezo. Kumbe ilikuwa kweli! Kauli yake ninaona imesimama. Ni mwele hakika. Laiti ningejua, jana ningeishi tofauti. Silesi zetu za maisha tungezila zilivyokuja kwa furaha. (Kimya). Siku hazigandiwala jana hairudi. Sasa jana imebaki kuwa kumbukizi baada ya kusombwa na wakati mfano wa mafuriko msimu wa masika. (Kimya). Kwa bahati nzuri bado tupo. Ninaweza kuiachia dunia tabasamu iwe silesi kwa vizazi vijavyo na kila mwenye nia njema. (Kimya). Siwezi kuendelea kuishi hivi. Sasa nimekata shauri. Lazima niache njia ya zamani na kuifuata mpya. Maisha mapya. Pombe! (kama anayeisemea pombe). Umenichezesha kama mwanasesere kwa muda mrefu. Umeninyima fursa ya kuielewa familia yangu. Hapana! Siku zangu za uzeeni lazima nizitumie kumwangalia mke wangu mgonjwa. Lazima nimshukuru kwa vitendo kwa jinsi alivyojitolea kuijenga familia yetu. (anapunga mkono.) Kwaheri pombe. Buriani.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

b) Bainisha toni ya dondoo hili.                                                                 (alama 2)

 

 

 

 

c) Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kuijenga tamthilia nzima.(alama 8)

 

 

 

 

 

6. 

               HADITHI FUPI

          Harubu ya maisha Paul Nganga Mutua

“Naja. Nakamilisha shughuli ndogo hapa kisha nianze safari…”

(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake                                                        (al. 4)

 

 

 

 

(b) Eleza sifa sita za msemaji wa kauli hii                                                            (al. 6)

 

 

 

 

 

 

(c) Jadili changamoto wanazokumbana nazo waajiriwa kwa kurejelea hadithi hii            (al. 10)

 

 

 

 

7. 

                                   HADITHI FUPI

              D.W .LUTOMIA    :  Msiba wa kujitakia  

Wetu ni wetu ,hata akiwa mbaya …ni wetu.hatuna budi kuchagua yeye .lisilobudi hubidi.

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.                            (alama 4)

 

 

 

 

(b) Fafanua vipengele vya kimtindo katika dondoo hii.            (alama 4)

 

 

 

 

(c) Hiari ya maamuzi ya wahusika mbalimbali yamewaletea madhila anuwai.jadili.(alama 12)

 

 

 

 

 

8. 

RIWAYA- NGUU ZA JADI

Hivyo,alitaka kubadili hali hata kama ilimaanisha kukitia kichwa chake kinywani mwa samba. Alitaka kuliokoa jahazi lililokuwa likielekea mwambani kwa kasi. Lakini angeliweza vipi kupambana na utandu wa mahasisi hao?.

(a) Eleza mbinu nne za mimtindozinazojitokeza katika dondoo  (al 4)

 

 

 

 

(b) Eleza sababu za msemaji kutaka kufaulisha kauli iloyopigiwa mstari   (al 10)

 

 

 

 

 

 

(c) Eleza umuhimu wa msemaji katika kujenga ploti ya riwaya hii  (al 6)