UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Mbuga ya Ziwa Nakuru, sasa imesafishwa katika mojawapo ya juhudi za kukabiliana na maji taka yanayoingia mbugani. Wasimamizi wa mbuga walitumia huduma za vijana wasiokuwa na ajira kutoka mitaa ya Bondeni, Kivumbini, Lake view, Free area na Flamingo kusafisha mito inayobeba uchafu huo.
Vibarua walizoa jumla ya tani 1.5, na baadaye tani 4.2 idadi inayofikisha zaidi ya tani 6.0 kwa siku mbili mfululizo.Hili linaashiria jinsi kina cha uchafuzi wa mazingira kwenye ziwa Nakuru umeshamiri,na baadhi ya wafanyikazi wanaona litajwe kuwa janga la kitaifa linalokodolea macho mbuga nyingi humu nchini.
Shughuli hiyo ilivutia hisia mseto huku maswali mengi kuliko majibu yakiibuka, endapo KWS ina bajeti ya kung’arisha mbuga za wanyama.
Akizungumza na Taifa Leo, mwangalizi wa utalii kutoka mbuga ya wanyama ya Ziwa Nakuru Bw Sirman Kioko, alisema maji taka yamekuwa yakiingia kwenye mbuga kutokana na miundo msingi duni. Aliongezea kuwa maisha ya wanyama hasa simba, nyati, vifaru, chui, viboko na flamingo yalikuwa hatarini,kwa sababu ya maji taka yalikuwa yamebadili mkondo na kupenyeza kwenye mbuga.
Miaka mitano iliyopita mbuga ya Nakuru ilikuwa na idadi kubwa ya ndege aina ya heroe ,lakini sasa wamebakia 200 tu. Hali hii itazidi kuwa mbaya,endapo idara husika haitaweka mikakati ya kutafuta suluhu la kudumu kwa wanyama pori wanaozidi kuangamia. Aidha uchafuzi katika ziwa Nakuru umefanya ndege kuhamia ziwa Bogoria ambapo inaaminika angalau chakula ni tele.
“Tunakubali kuwa gharama ya kusafisha mbuga ni kubwa,lakini pia tunaomba umma kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki inayoziba njia za maji,”alisema.
Pia aliongezea kuwa ni jukumu la mbuga kusafisha mazingira ya wanyama,lakini baraza la mji wa Nakuru pia lina nafasi kubwa ya kuhakikisha makazi ya watu ni safi,kwa kuzoa taka ipasavyo. Anaona kuna utepetevu mkubwa kutoka kwa usimamizi wa mazingira NEMA,wanaostahili kuweka sheria kali za kukabiliana na wale wanaoharibu mazingira. Aliongezea kuwa baraza la kusimamia huduma za wanyama pori (KWS),halina bajeti ya kusafisha mbuga na ndio sababu waliwaajiri vibarua saba kuendesha shughuli hiyo ya siku tatu. Uchafuzi wa mito inayoingia ziwa Nakuru hutokea msimu wa mvua ambapo maji hufurika na kusomba taka kutoka kwenye makazi ya watu.
Wanyama wanaovutia watalii kama vile Nyati hupata maradhi pindi wanapokunywa maji chafu,yaliyochanganyika na mifuko ya plastiki. Licha ya KWS kumiliki kituo cha kufanyia utafiti aina ya maradhi mbalimbali yanayokabili wanyama bado hawajafanikiwa kwa asilimia kubwa kuyazuia.
Hili linajiri siku moja tu baada ya wakazi wa mtaa wa Bondeni kuandamana barabarani wakilalamikia,ongezeko la kiwango cha takataka kwenye makazi ya watu.
(Imenukuliwa kutoka kwa Gazeti la Taifa Leo)
Maswali
a) Ipe taarifa hii kichwa mwafaka. (alama 1)
…………………………………………………………………………………………
b) Eleza sababu zinazofanya Ziwa Nakuru kuchafuka. (alama 2) ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………
c) Ni nini madhara ya kuchafuliwa kwa Ziwa Nakuru? (alama 4) ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………
d) Eleza vizingiti vinavyofanya ziwa hili kuendelea kuchafuliwa. (alama 2) ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………
e) Toa mapendekezo yanayoweza kusaidia kumaliza uchafuzi wa Ziwa Nakuru kulingana na taarifa hii. (alama 4) ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ………………..……………………………………………………………………………….
f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika taarifa. (alama 2)
i) Kupenyeza ………………………………………………………………………………………
ii) Utepetevu
……………………………………………………………………………………
Andika kisa kinachomalizikia kwa kauli ifuatayo:
…Tangu siku hiyo kijiji kizima kilipata funzo kwamba umdhaniaye ndiye kumbe siye na umdhaniaye siye kumbe ndiye.
Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
Wakosanao ndio wapatanao.
Mitandao ya kijamii ina faida na hasara zake. Thibitisha.
Wewe ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Upili ya Mamboleo. Mwanafunzi wako aliyefanya mtihani wake wa KCSE mwaka jana na kupita vizuri amepewa nafasi katika Chuo Kikuu cha Tumaini. Andika wasifu wake.
a) State three ways in which a person can become a member of parliament in Britain. (3marks)
b) Explain six functions of the president in India. (12marks)
a) State five common characteristics of the common wealth member state. (5marks)
b) Explain five ways through which United Nations promotes peace in the world. (10marks)
a) What were the results of the bombing of Nagasaki and Hiroshima in Japan in 1945. (3marks)
b) Describe six causes of the cold war. (12marks)
a) State five economic activities of the Asante during the 19th century. (5marks)
b) Describe the political organization of the Shona during the pre-colonial period. (10marks)
a) Give three methods used by European powers to establish colonial rule in Africa. (3marks)
b) Explain six effects of the British direct rule in Zimbambwe. (12marks)